Hujjatul Islam Dkt.Ali Taqavi ameeleza Leo la Kikao hiki cha Kielimu ni: Kufafanua mantiki ya ukabiliano wa kimfumo, wa kimaendeleo na wa kina, unaojengwa juu ya ufahamu wa ustaarabu wa Kiislamu na kurejea katika uwezo wa ndani wa ulimwengu wa Kiislamu, badala ya ukinzani wa kihisia au kauli mbiu zisizo na mizizi ya kielimu.

17 Oktoba 2025 - 12:46

Kikao cha Kielimu cha (Sisi na Magharibi) | Dr.Ali Taqavi: "Tunahitaji Ufahamu wa kina wa Ustaarabu wa Magharibi ili kuujibu kwa Misingi ya Kiislamu"

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwakilishi wa Jami‘at al-Mustafa (s) - Tawi la Dar es Salaam, Tanzania, Hujjatul Islam Dkt. Ali Taqavi, ametoa hotuba katika kikao cha awali cha kielimu kilichoandaliwa kwa lengo la kufungua upeo wa mazungumzo ya kitaaluma kuhusu haki halisi ya ustaarabu wa Magharibi na njia sahihi ya kukabiliana nao kwa mtazamo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sayyid Ali Khamenei (Allah Amhifadhi).

Kikao cha Kielimu cha (Sisi na Magharibi) | Dr.Ali Taqavi: "Tunahitaji Ufahamu wa kina wa Ustaarabu wa Magharibi ili kuujibu kwa Misingi ya Kiislamu"

Amesema kuwa lengo la kwanza la kikao hiki ni kuelewa misingi ya kifikra na kitambulisho cha ustaarabu wa Magharibi, kwani bila uelewa wa kina wa misingi hiyo, mtazamo wa Waislamu utabaki katika kiwango cha juu juu cha teknolojia na siasa pekee.

Kikao cha Kielimu cha (Sisi na Magharibi) | Dr.Ali Taqavi: "Tunahitaji Ufahamu wa kina wa Ustaarabu wa Magharibi ili kuujibu kwa Misingi ya Kiislamu"

Lengo la pili, amesema, ni kufafanua mantiki ya ukabiliano wa kimfumo, wa kimaendeleo na wa kina, unaojengwa juu ya ufahamu wa ustaarabu wa Kiislamu na kurejea katika uwezo wa ndani wa ulimwengu wa Kiislamu, badala ya ukinzani wa kihisia au kauli mbiu zisizo na mizizi ya kielimu.

Kikao cha Kielimu cha (Sisi na Magharibi) | Dr.Ali Taqavi: "Tunahitaji Ufahamu wa kina wa Ustaarabu wa Magharibi ili kuujibu kwa Misingi ya Kiislamu"

Hatimaye, kikao hiki kinalenga kufungua njia ya mazungumzo na ushirikiano wa kifikra kati ya wanazuoni wa vyuo vya dini na vya kisekula kuhusu mchakato wa ujenzi wa ustaarabu wa Kiislamu, kwani kwa mujibu wa mtazamo wa Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, ni kupitia ufahamu wa pamoja wa ustaarabu ndipo mfumo mbadala wa Kiislamu unaweza kuwasilishwa dhidi ya ustaarabu wa kimaada wa Magharibi.

Kikao cha Kielimu cha (Sisi na Magharibi) | Dr.Ali Taqavi: "Tunahitaji Ufahamu wa kina wa Ustaarabu wa Magharibi ili kuujibu kwa Misingi ya Kiislamu"

Mwisho wa hotuba yake, Dkt. Taqavi alionyesha matumaini kwamba kikao hiki kitakuwa mwanzo wa sura mpya ya uzalishaji wa fikra na maandiko ya kiustaarabu ndani ya ulimwengu wa Kiislamu.

Kikao cha Kielimu cha (Sisi na Magharibi) | Dr.Ali Taqavi: "Tunahitaji Ufahamu wa kina wa Ustaarabu wa Magharibi ili kuujibu kwa Misingi ya Kiislamu"

Your Comment

You are replying to: .
captcha